Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YAO NA WAARABU…YANGA WAANZIA MBALI…TAARIFA ZA CAF HIZI HAPA…

KUELEKEA MECHI YAO NA WAARABU…YANGA WAANZIA MBALI…TAARIFA ZA CAF HIZI HAPA…

Habari za Yanga

Kikosi cha Young Africans kimeanza maandalizi ya kuikabili CR Belouizdad ya Algeria katika mchezo wa Raundi ya Tano wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam, Februari 24.

Young Africans inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi D, sawa na vinara wa kundi hilo Al Ahly, lakini mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa wana mchezo mmoja mkononi dhidi ya Belouzidad yenye Pointi tatu utakaochezwa Algeria, Februari 16.

Kuelekea mchezo huo, Meneja wa Young Africans, Walter Harrison amesema wameamua kuanza maandalizi mapema lengo likiwa ni kushinda mchezo huo na kujiweka katika mazingira mazuri ya kwenda hatua ya Robo Fainali.

Amesema uongozi wa juu wa timu pamoja na Benchi la Ufundi chini ya Kocha Miguel Gamondi wamekuwa na vikao vya mara kwa mara vyenye lengo la kupata ushindi na kulipa kisasi cha mabao 3-0 waliyofungwa kwenye mchezo wa kwanza mjini Algiers, Algeria.

“Huu ni mchezo muhimu sana ambao kama tutashinda itakuwa tuna asilimia kubwa ya kutinga Robo Fainali bila kuangalia matokeo ya timu nyingine, ndio maana viongozi wa timu pamoja na Benchi la Ufundi wameanza mikakati ya ushindi mapema,” amesema Walter.

Meneja huyo amesema kwa sasa timu hiyo itakuwa inafanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni na watakuwa wanatokea nyumbani na wanatarajia kuingia kambini ikibaki wiki moja kabla ya mchezo huo.

Katika mechi nne ilizocheza Young Africans imeshinda mchezo mmoja, imetoka sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja.

SOMA NA HII  KOCHA WA VIUNGO SIMBA AFUNGUKA JINSI ALIVYOPATA ZALI LA KUAJIRIWA...ATOA SABABU ZA KUKATAA OFA ZA WAARABU...