Home Habari za michezo KABWILI AENDELEA KULIAMSHA YANGA…AIBUKA NA MADAI HAYA MENGINE…AWATAJA WANAOHUSIKA…

KABWILI AENDELEA KULIAMSHA YANGA…AIBUKA NA MADAI HAYA MENGINE…AWATAJA WANAOHUSIKA…


Mlinda Lango Ramadhan Kabwili amevunja ukimya na kueleza kwa undani ukweli wa maisha yake baada ya kushindwa kuonekana kwenye kikosi cha Young Africans msimu huu 2021/22, huku ikielezwa aliachwa mwishoni mwa msimu uliopita.

Kabwilia mbaye kwa kipindi kirefu alikua kimya amesema wadau wengi wa Soka la Bongo wamekua hawafahamu kinachoendelea kati yake na Uongozi wa Young Africans, lakini ukweli ni kwamba bado ni mchezaji halali wa klabu hiyo.

Mlinda Lango huyo aliyekua sehemu ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17 kilichoshiriki Fainali za Afrika 2017 nchini Gabon, amesema ni kweli hayupo kwenye kikosi cha Young Africans kwa muonekano, lakini yupo klabuni hapo na anaendelea kulipwa mshahara wake kila mwezi.

“Naomba niweke wazi leo bado nipo Yanga, napokea mshahara wangu kwa wakati na posho kama ilivyo kwa wachezaji wengine,”

“Kiukweli nimeamua kuweka wazi kwa sababu sio jambo dogo viongozi wangu wanalifanya, sipo ndani ya timu kwa maana ya kufanya mazoezi ila nipo kimkataba lakini wananipatia kila kitu kwa wakati.”

Mkataba wangu na Yanga umebaki wa miezi minne na mwisho wa msimu huu ndio utamalizika baada ya hapo nitawafuata na kuwauliza wapo tayari kuendelea na mimi au nitafute changamoto mpya sehemu nyingine.” amesema Kabwili

Kabwili alisajiliwa Young Africans msimu wa 2017/18 kama mchezaji huru na aliwahi kuaminiwa klabuni hapo chini ya Kocha Mwinyi Zahera kufuatia Mlinda Lango Claus Kindoki wa DR Congo kushuka kiwango.

Itakumbuka kuwa kwenye usajili wa dirisha dogo la mwezi wa kumi na mbili, Yanga walitangaza kuachana na Kabwili kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi, huku wakimsajili Mshery kutoka Mtibwa kuziba pengo lake.

SOMA NA HII  SABABU ZA YANGA KUACHANA NA LAMINE MORO IPO HIVI