Home Habar za Usajili Simba KUELEKEA MECHI DHIDI YA USGN….KIGOGO SIMBA ASHINDWA KUJIZUIA…ATOA AHADI HII YA AINA...

KUELEKEA MECHI DHIDI YA USGN….KIGOGO SIMBA ASHINDWA KUJIZUIA…ATOA AHADI HII YA AINA YAKE…


Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu ameahidi kutoa Tiketi 200 kwa Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo, kuelekea mchezo wa mwisho wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USGN ya Niger.

Simba SC itacheza dhidi ya USGN Jumapili (April 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam saa moja Usiku, huku ikihitaji ushindi wa aina yoyote ili kutinga Robo Fainali.

Mangungu ametoa ahadi hiyo kwa kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kwenye uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha Wanasimba kuelekea kwenye mchezo huo.

Akizungumza na Wanachama na Mashabiki wa Simba SC katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi Mwisho, jijini Dar es Salaam, Kiongozi huyo amesema atatoa tiketi 200, ili kuhamasisha wengine kununua tiketi za mchezo huo kwa wingi.

Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ limeipa Simba SC nafasi ya mashabiki 35,000 watakaoshuhudia mchezo dhidi ya USGN Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tayari Simba SC imeshaanza kuuza Tiketi za mchezo huo kwa njia ya Mtandao tangu juma lililopita, huku Wapinzani wao USGN wakitarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam alfajiri kesho Alhamis (Machi 31).

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKITUA MOROCCO JIONI HII...IBENGE AINGIA MCHEMCHETO...AJIAPIZA KUIHARIBIA..