Home Habari za Yanga KOCHA YANGA AMPIGA CHINI MCHEZAJI MMOJA…KIKOSI CHA KWANZA

KOCHA YANGA AMPIGA CHINI MCHEZAJI MMOJA…KIKOSI CHA KWANZA

NABI AONGEZEWA MKATABA YANGA...

Upo uwezekano mkubwa wa Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nasreddine Nabi kumuondoa beki mmoja wa kati katika kikosi chake cha kwanza na kumuingiza Ibrahim Hamad ‘Bacca’.

Mabeki wa kati wa Yanga ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job ambaye yeye katika mchezo wa juzi dhidi ya US Monastir alianzia benchi.

Wakati Bacca akimtoa beki huyo mmoja, Mamadou Doumbia raia wa Mali yeye bado anaendelea kupambana kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, kutoka katika benchi la ufundi la timu hiyo, ameliambia Championi Jumatano kuwa Nabi ameanza kumuingiza Bacca taratibu katika kikosi chake cha kwanza.

Bosi huyo alisema kuwa kocha anamuingiza katika kikosi chake kutokana uwezo mkubwa wa kuokoa, kupunguza hatari na kikubwa zaidi umahiri wake wa kucheza mipira ya juu golini kwao.

Aliongeza kuwa timu yao imekuwa na tatizo la kufungwa mabao ya mipira ya kona faulo kutokana na kutokuwepo beki mwenye uwezo kucheza mipira ya vichwa, hivyo anaamini Bacca ndio mkombozi wake kwa sasa.

“Tumekuwa tukifungwa mabao mengi ya mipira ya kutenga kwa maana ya kona, faulo na kona, hiyo imetokana na kumkosa beki wa kati mwenye umbile kubwa na uwezo wa kuicheza mipira ya vichwa.

“Hivyo Nabi amemfuatilia kwa karibu na kumuona Bacca anaja vizuri kuicheza mipira ya juu, hivyo amepanga kumtumia katika michezo ijayo ya ligi na kimataifa.

“Kuingia kwa Bacca katika kikosi cha kwanza kutamfanya beki mmoja kati ya Mwamnyeto na Job moja wao kupoteza namba, kwani hivi sasa kocha anamuongezea hali ya kujiamini ili acheze,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo Nabi alisema kuwa moja ya sababu ya kumuanzisha Bacca katika mchezo huu dhidi ya US Monastir, ni kuhitaji beki atakayecheza mipira ya vichwa.

“Katika mchezo huu dhidi ya US Monastir nilihitaji beki wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kucheza mipira ya vichwa na yeye nikaona anafaa baada ya kumuona mazoezini.

“Kwani aina ya mabao tuliyofungwa katika mchezo wa awali dhidi ya Monastir yametokana na uzembe wa mabeki kushindwa kuokoa mipira ya juu, na wao ni wapo vizuri kuicheza mipira ya aina hiyo,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  ENG. HERSI: YANGA TUKO TAYARI KUMWACHA FEI TOTO AENDE...VYUMA VINAKUJA ZAIDI...