Home Uncategorized KAMBI YA SIMBA YAVUNJWA AFRIKA KUSINI

KAMBI YA SIMBA YAVUNJWA AFRIKA KUSINI


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa kambi ya nchini Afrika Kusini imekuwa na mafanikio makubwa kwa sasa ni muda wa kuondoka Afrika Kusini.

Simba iliweka kambi nchini Afrika Kusini kwa muda wa wiki mbili ikiwa ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao leo wanarejea nyumbani baada ya kuivunja kambi.

Aussems amesema:- “Kwa sasa ni muda wa kuondoka Afrika Kusini baada ya kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

“Tumeifanya kwa mafanikio makubwa na juhudi kubwa hivyo shukrani zetu kwa wote waliokuwa nasi,”.

SOMA NA HII  REKODI ZA MESSI NA BARCELONA, KWA SASA HATAKI KABISHA KUBAKI HAPO