Home Uncategorized SHINDA GARI SASA YAFIKA PATAMU, MSHINDI NJIANI KUPATIKANA

SHINDA GARI SASA YAFIKA PATAMU, MSHINDI NJIANI KUPATIKANA


LILE shindano la wasomaji wa magazeti bora ya michezo zilizofanyiwa uchunguzi wa kina, Championi na Spoti Xtra, ambapo mshindi anatarajiwa kukabidhiwa gari jipya aina ya Toyota FunCargo sasa linaelekea ukingoni kwa ajili ya mshindi kukabidhiwa ndinga hiyo.

Jana Alhamisi, Kitengo cha Masoko na Usambazaji cha magazeti hayo, kilitua mitaani maeneo mbalimbali ya Tegeta jijini Dar kwa ajili ya kuendelea kuwahamasisha wasomaji hao kuzidi kununua magazeti hayo na kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili wa magazeti hayo kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu hiyo.

Akizungumza na wasomaji hao Mkuu wa Kitego hicho, Anthony Adam aliwaambia wasomaji hao wazidi kushiriki shindano hilo kwani gari hiyo inatarajiwa kukabidhiwa kwa mshindi mapema mwezi ujao.

SOMA NA HII  WALTER BWALYA AIPA TANO SIMBA KWA KAHATA