Home Habari za Yanga USAJILI YANGA: YAMFUATA MSHAMBULIAJI RASTA…NABI ASISITIZA

USAJILI YANGA: YAMFUATA MSHAMBULIAJI RASTA…NABI ASISITIZA

Habari za Yanga SC

Wakati mabosi wa timu ya Ihefu FC, wakiendelea kujiridhisha na
uwezo wa straika wao mwenye rasta raia wa Burkina Faso, Yacouba Sogne, mabosi wake wa zamani Yanga, wanadaiwa kurejesha nia ya kumsajili kwenye dirisha kubwa lijalo ili akaongeze nguvu kwa Fiston Mayele na Kennedy Musonda.

Tangu ajiunge na Ihefu, Yacouba amefanikiwa kufunga mabao mawili na kutoa asisti moja huku akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Februari.

Yacouba alijiunga na Ihefu kwenye dirisha dogo mwaka huu kama mchezaji huru akitokea Yanga kufuatia kukosa nafasi katika kikosi cha kocha Nasraddine Nabi, mara baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha yaliyomuweka nje karibia mwaka mzima.

Chanzo chetu kutoka Yanga kimesema kwamba, tayari mabosi wa timu hiyo wameonyesha hali ya kuvutiwa na kuimarika kwa Yacouba jambo linalowafanya kumuita mezani upya ili wamrejeshe kikosi msimu ujao huku Ihefu nao wakiweka ngumu kumuachia.

“Kufuatia maelekezo ya kocha Nabi, kuna uwezekano tena wa kumrejesha Yacouba kikosini mwetu msimu ujao, maana tayari anaona mwenendo wake unamvutia na kwamba amesema yawezekana akaja kuongeza nguvu kikosini katika upande wa washambuliaji,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kumtafuta Kocha wa Ihefu, Zubeir Katwila ambapo alisema: “Kwa sasa bado tupo kwenye maboresho ya kikosi chetu, hivyo

SOMA NA HII  IMEVUJA RASMI...KIPA KINDA SIMBA AWEKEWA ULINZI MZITO...ISHU KAMILI A-Z HII HAPA