Home Simba SC SIMBA YASAJILI MTAMBO WA MABAO 9

SIMBA YASAJILI MTAMBO WA MABAO 9


NYOTA Mpya wa Simba, Yusuph Mhilu kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia jumla ya mabao 9 kati ya 38 ambayo yalifungwa na timu hiyo.

Alikuwa ni namba moja kwa utupiaji na bao lake la kwanza alifunga mbele ya KMC, ilikuwa Uwanja wa Kaitaba zama za Mecky Maxime ambaye alichimbishwa mazima kazi ndani ya timu hiyo.

Kwa sasa Mhilu ni mali ya Simba ambapo alikuwa anatajwa pia kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Yanga mambo yakawa tofauti baada ya mabosi wa Simba kumpa dili la miaka miwili.

Unakuwa ni usajili wa pili kwa Simba msimu huu baada ya ule wa kwanza wa Peter Banda kutangazwa na sasa ni zamu Mhilu.

Nyota huyo ndani ya Kagera Sugar ameyeyusha jumla ya dakika 2,142 alizocheza kwenye Ligi Kuu msimu wa 2020/2021 kati ya mechi 34 ambazo timu hiyo ilicheza.

Kwenye msimamo timu ya Kagera Sugar ilimaliza ikiwa nafasi ya 12 na pointi zake 40 inanolewa na Kocha Mkuu Francis Baraza.
SOMA NA HII  DAKIKA KADHAA KABLA YA KUKIPIGA NA AL AHLY...MASTAA SIMBA WALA KIAPO CHA KUFA KUPONA..