Home Habari za michezo DAKIKA KADHAA KABLA YA KUKIPIGA NA AL AHLY…MASTAA SIMBA WALA KIAPO CHA...

DAKIKA KADHAA KABLA YA KUKIPIGA NA AL AHLY…MASTAA SIMBA WALA KIAPO CHA KUFA KUPONA..

FT:SIMBA 2-2 AL AHLY

Simba inapaswa kuwa na nidhamu kubwa hasa ya kujilinda ili kuhakikisha Al Ahly hawana madhara makubwa kwao na wao waweze kupata matokeo mazuri yatakayowavusha.

Uimara wa hali ya juu unapaswa kuwepo katika safu ya kiungo ambayo imekuwa ikifanya makosa ya mara kwa mara ya kuruhusu wapinzani kumiliki mpira na kutengeneza nafasi, jambo linalopelekea safu ya ulinzi ishambuliwe mara kwa mara.

Wawakilishi hao wa Tanzania wanapaswa kutimiza wajibu kitimu hasa kukaba na kutafuta mpira pindi unapokuwa kwa Al Ahly, jambo ambalo litawanyima uhuru wapinzani wao katika kutengeneza hatari kwao.

Kuepuka makosa binafsi ya kiulinzi kunaweza kuwa msaada mkubwa kwa Simba ambayo siku za hivi karibuni imeonekana kuruhusu idadi kubwa ya mabao kutokana na uzembe binafsi.

Wakati huo huo, mastaa Simba wamepania kuitoa wapinzani wao kwao, Simba inahitaji ushindi au sare yoyote ya mabao kuanzia 3-3 kusaka nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na mabingwa hao wa Afrika katika mchezo wa kwanza.

Mfungaji wa bao la kwanza la Simba kwenye mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa kwa Mkapa Ijumaa iliyopita, Kibu Denis amesema β€œAhly ni timu kubwa lakini hata sisi ni wakubwa, kila kitu kinawezekana kwenye soka. Tuna timu nzuri na kila mchezaji anajituma huku tukiwa na ushirikiano wa kutosha.”

β€œZitakuwa ni dakika 90 za nguvu, tutapambana hadi mwisho na lengo ni kutinga nusu fainali.”

Wakati Kibu akiyasema hayo naye beki wake wa kulia Shomari Kapombe amesisitiza akisema wanahitajika kuipa presha safu ya ulinzi ya waarabu hao ambayo inafanya makosa.

“Mabao mawili ambayo wameyaruhusu kwenye mchezo mmoja dhidi ya yetu ndio mabao ambayo waliyaruhusu ndani ya mechi zao tisa zilizopita hapa maana yake tunatakiwa kuwa sawa kwenye usham-buliaji kwa kuwa safu yao ya ulinzi inafanya makosa,”amesema Kapombe.

SOMA NA HII  BENCHIKHA AREJESHA MATUMAINI MAPYA SIMBA