Home Uncategorized NYOTA STARS AENGULIWA MOJAKWAMOJA KAMBINI

NYOTA STARS AENGULIWA MOJAKWAMOJA KAMBINI

MUDHATHIR Yahya sasa hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kifundo cha mguu.

Timu ya Taifa ya Tanzania ipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Chan na mchezo wake wa kwanza ni Julai 28 dhidi ya Kenya Uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Juma Mgunda amesema kuwa wameamua kumpa mapumziko moja kwa moja mchezaji huyo ili apate matibabu.

“Mudhathiri hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kwa kuwa hali yake haipo imara, ataendelea kupata matibabu ili kutengamaa na kureea kwenye ubora wake,” amesema.

Mudhathiri alipata maumivu hayo kwenye timu ya Taifa ya Tanzania wakati wa michuano ya Afcon nchini Misri hakushiriki pia michuano ya Kagame iliyofanyika nchini Rwanda.

SOMA NA HII  SERIKALI YAFIKIRIA KUREJESHA LIGI ZOTE NCHINI