Home Ligi Kuu COASTAL UNION: ILIKUWA MIPANGO YA MUNGU KUIFUNGA YANGA

COASTAL UNION: ILIKUWA MIPANGO YA MUNGU KUIFUNGA YANGA


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa ushindi wake mbele ya Yanga ni mipango ya Mungu kwa kuwa yeye ni muweza wa yote.

Jana, Machi 4 ilikuwa ni vita ya kibabe Uwanja wa Mkwakwani, dakika 90 ubao ulisoma Coastal Union 2-1 Yanga.

Ushindi huo unaifanya Coastal Union kuwa timu ya kwanza kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Yanga ya Yanga Cedric Kaze ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza msimu wa 2020/21.

Mgunda amesema kuwa hawakuwa na namna ya kufanya ila mpango wa Mungu ulitimia.

“Hakukuwa na namna ya kufanya kwani vijana wangu niliwaambia kwamba mchezo utakuwa mgumu wanapaswa wapambane ndani ya uwanja.

“Mungu amejibu maombi yetu nasi tumeshinda hivyo ni fuaraha kwetu na mashabiki wetu, mapambano bado yanaendelea,” amesema. 

SOMA NA HII  WAKALI WA KUCHEKA NA NYAVU BONGO HAWA HAPA