Home Uncategorized RUVU SHOOTING: TUNAKIWASHA KWA KASI MSIMU UJAO

RUVU SHOOTING: TUNAKIWASHA KWA KASI MSIMU UJAO

UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa msimu ujao utapambana kupata matokeo chanya kwenye ligi tofauti na msimu uliopita.

Ruvu Shooting imeweka kambi mkoani Pwani na ipo chini ya Kocha Mkuu, Salum Mayanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwre amesema kuwa hesabu kubwa zipo kwenye kuleta ushindani mkubwa.

“Msimu ujao tunahitaji kuleta ushindani mkubwa na tumejipanga kufanya vizuri, kwa sasa tayari tumeingia kambini lengo kujenga kikosi imara,” amesema.

Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza Agosti 23 na mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya Simba na JKT Tanzania uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  MTUPIAJI LIGI KUU BARA AMTAJA BOCCO WA SIMBA KUWA MCHEZAJI HATARI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here