Home Azam FC SURE BOY, MORRIS MAMBO SAFI

SURE BOY, MORRIS MAMBO SAFI

 


HABARI njema kwa kikosi cha klabu ya Azam ni kurejea kwa nyota wao wawili waliokuwa na majeraha, Salumu Abubakar ‘Sure Boy’ na Aggrey Morris.

Sure Boy na Morris walipata majeraha hayo katika mazoezi ya kikosi chao kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC, mchezo iliopigwa siku ya Jumamosi.

Azam jana ilicheza dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa kimataifa wa Kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam na kushuhudua Azam ikilazimishwa sare ya bao 1-1.

Akizungumzia hali za nyota hao Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema nyota hao tayari wamefanya mazoezi ya pamoja na wenzao.

“Ni kweli wachezaji wetu wawili, Sure Boy pamoja na nahodha, Aggrey Morris walipata majeraha katika maandalizi yetu kuelekea mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya KMC.

“Lakini hayakuwa majeraha makubwa kwani tayari wamerejea uwanjani na kufanya mazoezi ya pamoja na timu,”

SOMA NA HII  BAADA YA KUWABUTUA YANGA...KOCHA AZAM FC AWAVUTIA KASI YA MBALI SIMBA...