Home Uncategorized WAWA: NINAONDOKA BONGO

WAWA: NINAONDOKA BONGO

BEKI kisiki wa Simba mwenye mwili uliojengeka kimazoezi Pascal Wawa amesema kuwa kwa sasa anatarajia kuondoka bongo muda wowote kuelekea nchini Ivory Coast kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa baada ya kutwaa ubingwa ndani ya kikosi cha Simba ni muda mwafaka kwake kusepa kwenda nyumbani kupumzika ili kujiandaa kwa msimu ujao.

“Nashukuru, kwa kushirikiana na wenzangu tumebeba ubingwa hilo lilikuwa ni jambo kubwa na la msingi, kilichobaki kwa sasa ni kuondoka kurejea nyumbani kuiona familia yangu.

“Sitakaa sana hapa bongo inanibidi niondoke kwa kuwa nilikuwa ninamajukumu namalizia ila kwa sasa nitaondoka kwa ajili ya kupumzika,” amesema Wawa ambaye amecheza jumla ya michezo 21 ndani ya Simba.

SOMA NA HII  ISHU YA BILIONI MOJA YA MAGUFULI YAMVUTA KIGOGO TAKUKURU