Home Uncategorized MLINZI WA SHULE ALIYEMUUA MWANAFUNZI AHUKUMIWA KIFO

MLINZI WA SHULE ALIYEMUUA MWANAFUNZI AHUKUMIWA KIFO


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Moshi imemhukumu kunyongwa hadi kufa mlinzi wa Shule ya Sekondari ya Scolastica, Hamis Chacha (30), baada ya kupatikana na kosa la kumuua mwanafunzi Humprey Makundi (16).

Aidha, mahakama hiyo imewahukumu watuhumiwa wengine ambao ni mmiliki wa shule hiyo, Edward Shayo (65),  na aliyekuwa mwalimu wa zamu, Labani Nabiswa (39) raia wa Kenya, miaka minne jela kila mmoja kwa kosa kuficha ukweli wa mauaji hayo.

Mwili huo uliokaa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa zaidi ya siku 14 kabla ya kuzikwa katika kijiji cha Mamba kwa Makundi ,Marangu wilaya ya Moshi kutokana na kutoka kwa majibu ya sampuli ya vina saba (DNA) ikionyesha kuwa mwili ni wa Humphrey Makundi.

Novemba  6, 2017 taarifa za kutoweka kwa mwanafunzi huyo katika shule aliyokuwa akisoma ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo zilianza kuzagaa katika mitandao ya kijamii na baadae Novemba 7 huo mwili ulikutwa ukiwa umetelekezwa mto Ghona unaokadiliwa kuwa mita 300 kutoka katika shule hiyo.

Mwili huo ambao awali ulifikishwa katika Hosptali ya mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi ulipokelewa na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti na baadae kuzikwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi katika makaburi ya Karanga kama mwili usiokuwa na ndugu.

Hata hivyo, baada ya kuwepo kwa taarifa ya kuzikwa kwa mwili huo, familia ya Makundi iliomba kibali cha mahakama kuruhusu  kufukuliwa mwili huo kwa lengo la kujiridhisha, mtu aliyezikwa kama kweli ni mzee kama taarifa za awali zilivyotolewa au ni ndugu yao.

Watuhumiwa watatu walishikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi huyo na katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Moshi na kusomewa shtaka la mauaji mbele ya Hakimu Mkazi, Julieti Mawore na wakili wa serikali Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea, Faygrace Sadallah huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Eliakunda Kipoko.

SOMA NA HII  MO AZUIA JARIBIO YANGA