Home Uncategorized POLISI TANZANIA YAPANIA KUPAMBANA TPL

POLISI TANZANIA YAPANIA KUPAMBANA TPL


UONGOZI wa kikosi cha Polisi Tanzania umesema kuwa kwa sasa hesabu kubwa ni kujipanga kisawasawa kwa ajili ya msimu wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara hivyo wanaanza na usajili makini utakaowafanya wawe imara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa kwa sasa wanaifanyia kazi ripoti ya kocha ambayo ndiyo muongozo kwa watakaowasajili.

“Ripoti imeshatua na tumeanza mikakati makini ambayo itatufanya tuwe bora na tushindane na timu zote ndani hivyo kama ambavyo tulipambana kupanda ligi kuu ndivyo ambavyo tutapambana ndani ya ligi,” amesema.

SOMA NA HII  MOSES PHIRI NGOMA NGUMU SIMBA