Home news DAKIKA KADHAA KABLA YA KARIAKOO DABI…BARBARA AIBUKA NA JIPYA KUHUSU MORRISON NA...

DAKIKA KADHAA KABLA YA KARIAKOO DABI…BARBARA AIBUKA NA JIPYA KUHUSU MORRISON NA MKUDE…


OFISA mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amewaita mashabiki wa timu hiyo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kuishangia chama lao.

Barbara amesema asubuhi ya leo alikuwa kambini alipata nafasi ya kuongea na wachezaji pamoja na benchi la ufundi umhimu wa mechi hiyo ni kubwa ndani na nje ya Afrika.

Amesema baada ya mazungumzo hayo alipata kifungua kinywa nao kwa pamoja.

“Wachezaji kama Jonas Mkude, Benard Morrison na wengine wote waliokuwa kambini wapo fiti na morali ya hali ya juu kwa ajili ya kuipigania Simba na kupata pointi tatu,” amesema Barbara na kuongeza;

“Ukimuangalia kila mchezaji katika kambi yetu yupo na hamu ya hali ya juu kupata nafasi ya kucheza ili kwenda kuipagania timu kupata ushindi kama malengo yalivyo.”

“Kila shabiki na mpenzi wa Simba natamani kusikia huko alipo anajiandaa kwenda uwanjani akiwa na hali kubwa ya kwenda kuipa nguvu timu yetu na kuishangilia mwanzo mwisho.

“Binafsi nipo katika maandalizi ya mwisho kwenda Uwanjani ili kushirikiana na mashabiki wetu katika kuwapa nguvu wachezaji na benchi la ufundi.”

SOMA NA HII  HAPA SIMBA PALE YANGA HII NDIO LIGI YA REKODI SASA