Home Uncategorized BEKI SIMBA ATAJWA NDANI YA COASTAL UNION

BEKI SIMBA ATAJWA NDANI YA COASTAL UNION

IMEELEZWA kuwa beki wa kati wa Yusuph Mlipili ameingia anga za Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu,  Juma Mgunda. 


Mlipili ambaye aliachwa na Simba msimu uliopita kutokana na kukosa nafasi kikosi cha Kwanza ni miongoni mwa wazawa mwenye uwezo mkubwa akiwa ndani ya uwanja.


Ujio wa Joash Onyango na Pascal Wawa ambao ni mabeki wa kati uliongeza ufinyu wa namba kikosi cha Kwanza jambo lililofanya nyota huyo apigwa chini mazima licha ya uwezo wake.


 Mgunda ameweka wazi kwamba moja ya sehemu ambayo ataifanyia maboresho ni sehemu ya beki kwa kuwa baada ya kuondoka kwa pacha ya Bakari Mwamnyeto anayekipiga Yanga na Ibrahim Ame ndani ya Simba mambo yamekuwa magumu.


Kwa msimu wa 2020/21 inashikilia rekodi ya kufungwa mabao mengi ambayo ni 7-0 ilifungwa na Simba, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.


Mgunda amesema:”Ni lazima nifanyie maboresho safu yangu ya ulinzi na ushambuliaji Kwenye dirisha dogo hivyo mipango ikikamilika kila kitu kitawekwa wazi,”.

SOMA NA HII  POGBA MZINGUAJI KINOMA, ALIANZISHA KAMBINI