Home Uncategorized KUMBE LEGENDI HENRY HAMUELEWI XHAKA

KUMBE LEGENDI HENRY HAMUELEWI XHAKA

 


NYOTA wa zamani wa Klabu ya Manchester United zama za Sir Alex Ferguson, Patrice Evra aliyezaliwa Senegal raia wa Ufaransa amesema kuwa Legendi wa zamani wa Arsenal,  Thiery Herny alizima TV timu yake ilipokuwa ikicheza.


Evra amesema kuwa siku moja aliwahi kualikwa nyumbani kwa Henry wakati timu yake ilipokuwa ikicheza ila muda mfupi baada ya kuwasha TV na kuona timu yake ikicheza alizima ghafla TV baada ya picha ya kwanza kuonyesha Granit Xhaka akiwa ni nahodha. 


Nyota huyo alipomuuliza Henry sababu ni nini aliambiwa wazi kuwa hawezi kutazama mchezo wa timu yake ya zamani huku nahodha akiwa ni Xhaka na hawawezi kuangalia mchezo huo.


Arsenal ambayo imekuwa na mwendo wa kusuasua ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Burnley ikiwa nyumbani Uwanja wa Emirates kwa bao la kujifunga la nahodha Pierre Emerick Aubameyang dk 73.


Kwenye mchezo huo dakika ya 56 nahodha wa zamani wa kikosi hicho Xhaka alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea faulo Ashley Westwood.


Kwenye msimamo ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 13 imepoteza jumla ya mechi 7 baada ya kucheza mechi 12 na Burnley ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 9 baada ya kucheza mechi 11 kinara ni Tottenham mwenye pointi 25.

SOMA NA HII  HUU HAPA MUONEKANO MPYA WA UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR