Home Habari za michezo KOCHA YANGA ANUKIA MSIMBAZI….NI YULE ALIYEAGWA JUZI….NAFASI YAKE SIMBA IKO WAZI…

KOCHA YANGA ANUKIA MSIMBAZI….NI YULE ALIYEAGWA JUZI….NAFASI YAKE SIMBA IKO WAZI…

Tetesi za Usajili Simba

BAADA ya mabosi wa Simba kuachana na Chlouha Zakaria aliyekuwa kocha wa makipa jina la kocha wa Yanga, Milton Nienov linatajwa mitaa ya Msimbazi.

Juni 15 Simba imebainisha kuachana na kocha huyo ambaye alikuwa anawanoa Aishi Manula kipa namba moja wa Simba, Beno Kakolanya kipa namba mbili pamoja na Ally Salim ambaye ni kipa namba tatu.

Milton raia wa Brazil ana uzoefu na ligi ya Bongo na aliwahi kuwanoa makipa hao ndani ya Simba lakini alisitishiwa mkataba wake kutokana na timu kuboroga kwenye anga za kimataifa kisha akaibukia Yanga.

Taarifa zinaeleza kuwa miongoni mwa makocha ambao wanatazamwa kupewa mikoba ndani ya Simba ni kocha huyo anayewanoa makipa wa Yanga iliyogotea hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mbali na kocha wa makipa ni Kelvin Mandla kocha wa viungo, Fareed Cassim ambaye ni mtaalamu wa viungo pamoja na Charlse Lukula huyu alikuwa Kocha Mkuu wa Simba Queens ambayo imeyeyusha ubingwa wao uliochukuliwa na JKT Queens naye amepewa mkono wa kwa kheri.

SOMA NA HII  KISA SIMBA KUANZIA NYUMBANI NA YANGA UGENINI..BODI LA LIGI WAIBUKA NA KUTOA KAULI HII YA JUMLA...