Home news BAADA YA SIMBA KUCHAPWA NA KAGERA JUZI…PABLO ATIKISA KICHWA KISHA ASEMA HAYA…ADAI...

BAADA YA SIMBA KUCHAPWA NA KAGERA JUZI…PABLO ATIKISA KICHWA KISHA ASEMA HAYA…ADAI KUUMIA…


KOCHA Mkuu wa Timu ya Simba, Franco Pablo Martin amewaomba radhi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kufuatia kichapo cha 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Simba ilipoteza mchezo huo mkoani Kagera, juzi Jumatano bao likifungwa na Khamis Kiiza ‘Diego’. Kocha Pablo amesema imekua bahati mbaya kwa kikosi chake kupoteza mchezo huo, hivyo hana budi kuomba radhi kwa kilichotokea Uwanja wa Kaitaba.

“Ni matokeo ya kusitikisha sana, hatukutarajia kwa sababu tulijiandaa kushinda, imeniuma sana kupoteza alama tatu hapa, niwateke radhi Mashabiki ambao walikua na matumaini na timu yao leo (jana),” amesema Pablo.

Simba imepoteza mechi mbili msimu huu na sare nne, hivyo kuwa nyuma kwa pointi 10 nyuma ya Yanga wanaoongoza Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  SIMBA vs AS VITA | GOMES - TUNAKUJA KIVINGINE