Home news PAMOJA NA KUWA NA KUWANGO KIKUBWA…NABI APITISHA ‘TIKI YA KIJANI KWA SAIDO’…UONGOZI...

PAMOJA NA KUWA NA KUWANGO KIKUBWA…NABI APITISHA ‘TIKI YA KIJANI KWA SAIDO’…UONGOZI WATOA NENO…


SASA uhakika kiungo mshambuliaji wa Yanga Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ raia wa Burundi, ataendelea kuichezea timu hiyo katika msimu ujao, hii ni baada ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kutaka aongezewe mkataba.

Mrundi huyo ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Wengine baadhi ni Dickson Job, Kibwana Shomari, Bakari Mwamnyeto, Deus Kaseke na Farid Mussa.

Kwa siku za karibuni, kiungo huyo ameonekana kurejea kwa kasi akionesha kiwango bora na kumfanya aingie kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, amesema kuwa, Kocha Nabi ameridhishwa na kiwango kikubwa ambacho amekionesha Saido kwa siku za karibuni.

Bosi huyo alisema Nabi mara baada ya mchezo wa Polisi Tanzania, haraka aliwaambia viongozi wa timu hiyo, wamuongezee mkataba wa kuendelea kukipiga hapo.

Aliongeza kuwa, kocha huyo bado anaendelea kuwatazama baadhi ya wachezaji wengine ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu kwa ajili ya kupendekeza usajili wao.

“Kocha Nabi ndiye anayependekeza usajili wote wa timu, hivyo kama yeye akipendekeza mchezaji fulani asajiliwe, basi hakutakuwa na pingamizi lolote kwa uongozi. “Hivyo Saido jina lake limependekezwa na Nabi ambaye amewaomba viongozi aongezewe mkataba wa kuendelea kuichezea Yanga.

“Ni suala la muda tu, hivyo muda wowote atapewa mkataba mpya mara baada ya kukaa meza moja na viongozi kwa ajili ya kufanya mazungumzo,” alisema bosi huyo.

Akizungumzia hilo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema: “Kila kitu kinachohusiana na usajili tumemuachia kocha, hivyo bado hatujakutana na kocha kujadiliana usajili.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA WAARABU...MSUVA AZIITA SIMBA NA YANGA...AZAM HUENDA WAKAFANYA KWELI...