Home Uncategorized SADIO MANE APELEKA MAUMIVU KWA WESTHAM UNITED, LIVERPOOL BALAA

SADIO MANE APELEKA MAUMIVU KWA WESTHAM UNITED, LIVERPOOL BALAA


SADIO Mane, mshambuliaji wa Liverpool raia wa Senegal alitimiza majukumu yake Jana wakati wakiilaza kwa mabao 3-2 Westham United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.


Bao la kwanza la kuongoza lilifungwa na Georginio dakika ya 9 lilisawazishwa na Westham dakika ya 12 kupitia kwa Issa Diop na dakika ya 54 Westham wakiwa Anfield wakiongeza bao la pili kupitia kwa Pablo Fornals lilisawazishwa dakika ya 68 na Mohamed Salah.

Westham wakiamini watasepa na pointi tatu, dakika tisa kabla ya mpira kukamilika Sadio Mane alifunga bao la ushindi dakika ya 81 na kuipa pointi tatu timu yeke.

Liverpool inafikisha jumla ya pointi 79 ikiwa nafasi ya kwanza na Westham ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 24 zote zimecheza mechi 27.

SOMA NA HII  UJUMBE HUU WA ALLIANCE WATUMWA YANGA