Home news SONSO AJIFUNGA MWAKA MMOJA NDANI YA RUVU SHOOTING

SONSO AJIFUNGA MWAKA MMOJA NDANI YA RUVU SHOOTING

KAZI imeanza kwa mabosi wa Ruvu Shooting baada ya kumpa dili la mwaka mmoja Ally Mtoni, ‘Sonso’ mkataba wa mwaka mmoja.
Nyota huyo alikuwa anakipiga ndani ya Kagera Sugar na hakuongezewa kandarasi nyingine baada ya dili lake kuisha jambo lililompa urahisi, Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa kumpata mchezaji huyo.
Mkwasa anamtambua vema Sonso kwa kuwa aliwahi kufanya naye kazi alipokuwa ndani ya kikosi cha Yanga kwa nyakati tofauti ataungana na Mohamed Issa, ‘Banka’ ambaye naye aliwahi kucheza Yanga na sasa yupo na Mkwasa ndani ya Ruvu Shooting.
Hivi karibuni Ofisa Habari wa Ruvu Shooting aliliambia Championi Jumamosi kuwa watasajili kwa umakini na kuzingatia ripoti ya mwalimu.
Kwenye msimamo Ruvu Shooting ilimaliza ikiwa nafasi ya 11 ikiwa na pointi 41 baada ya kucheza mechi 34 ilikuwa haina mwendo bora msimu uliopita wa 2020/21 jambo ambalo limewafanya mabosi wa timu hiyo kupiga hesabu za kujipanga zaidi.

 

SOMA NA HII  KIMEUMANA SIMBA...PABLO ATAKA MASHINE MPYA TATU...MATOLA NA HITIMANA HATIHATI KUSALIA...