Home kimataifa MANCHESTER UNITED BADO WANAAMINI WATAMPATA HAALAND

MANCHESTER UNITED BADO WANAAMINI WATAMPATA HAALAND


 MANCHESTER United inaamini kwamba itafanikiwa kuipiga bao Chelsea kwa kumpata staa wa Borussia Dortmund, Erling Haaland.

Haaland kwa sasa amekuwa akitajwa kuwa huenda akajiunga na United ama Chelsea ambazo zimekuwa zikiwania saini yake.

United walikuwa wanahitaji kumpata nyota huyo tangu alipokuwa RB Salzburg lakini ikashindikana, Januari 2020 akatua ndani ya Dortmund alipo kwa sasa.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer anaamini kwamba atampata mshambuliaji huyo na amekuwa akiwasiliana naye mara kwa mara.

Chelsea wao wapo tayari kuweka dau la pauni milioni 150 kupata saini ya nyota huyo huku United wao wakiamini kwamba kama watamkosa msimu huu basi watakomaa kuipata saini yake msimu ujao. 

SOMA NA HII  POCHETTINO ATAJWA SPURS