Home Makala U 23 MNASTAHILI PONGEZI, KAZI INAENDELEA KWA WAKUBWA

U 23 MNASTAHILI PONGEZI, KAZI INAENDELEA KWA WAKUBWA


 WAKATI mwingine tena ambao vijana wetu wa Tanzania wamefanya vizuri. Ilikuwa ni kwenye Cecafa U 23 iliyofanyika nchini Ethiopia.

Kwa juhudi ambazo wamezifanya na kazi kubwa iliyofanywa kwa vijana wetu wanastahili pongezi kubwa. Lakini wasisahau kwamba lazima waendelee kufanya vizuri kwenye mashindano mengine.

Muda huu ni wa furaha kwa Tanzania kiujumla pamoja na wachezaji. Benchi la ufundi limetimiza majukumu yao na kufanya kazi ile ambayo ilistahili basi pongezi muhimu.

Kazi ni moja kwao kupambana kuendelea kutimiza majukumu yao kwa kuwa wakati uliopo ni sasa na kikubwa ni maandalizi mazuri na kufanya kazi kwa ushirikiano.

Ukirejea kwenye ligi tayari ni timu nyingi zipo kwenye mapumziko kwa sasa na nyingine zimeanza kushiriki mashindano ya Kagame.

Na kuna jambo la usajili kwa kuwa dirisha limefunguliwa hivyo yote ni muhimu kwenda nayo kwa wakati huu bila kuacha jambo kwa kuwa yote ni yetu sote.

Katika usajili umakini na uhitaji ni mambo ya kuzingatia ili kupata wachezaji ambao watafanya vizuri watakapopata nafasi ya kuzitumikia timu mpya.

Jambo la msingi kwa timu ambazo zinashiriki Kagame kufanya kazi kwa juhudi. Muhimu ni kuona kwamba ushindi unapatikana.

Nina amini kwamba kila timu ambayo inaiwakilisha Tanzania inatambua kwamba mashabiki wanahitaji ushindi na inawezekana kwa kujituma bila kuogopa.

Ndani ya dakika 90 ni muda sahihi uwanjani ambao utatosha kuaminisha mashabiki na wanachama wa timu kwamba wapo uwanjani kupambana kupata ushindi.

Mashabiki nao wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kutoa sapoti kwa wachezaji wa timu zao ili kupata matokeo mazuri. Kila mchezaji anatambua kwamba kitu ambacho mashabiki wanahitaji ni matokeo.

Kuwa nyumbani ni moja ya fursa ambayo inapaswa itumike kwa timu shiriki kupambana kwa hali na mali katika kusaka matokeo.


Inawezekana kushinda na kupata taji kwa mechi ambazo zitachezwa nyumbani. Jambo la msingi ni kufanya maandalizi mazuri ili kupata matokeo chanya.

Kwa wale wachezaji ambao wamepata bahati ya kuwa kwenye maisha mapya basi wana kazi ya kuonyesha kile kitu ambacho wanacho kwenye mashindano haya.

Nyingine zinatumia wachezaji kutoka timu ya vijana hili ni jambo zuri kwao ikiwa watapambana kusaka matokeo. Wakati wao wa kuonekana utakuwa ni sasa ili waweze kuzitimiza ndoto zao.

Kwa muda huu ambao timu nyingine zimetoa mapumziko iwe hivyo kwa wachezaji wote kupata muda wa kuwa na ndugu na jamaa pamoja na familia.

Kila mtu atavuna kile atakachokipanda ndani ya uwanja ni wakati wa kuanza maandalizi kwa timu zote kwani muda wa ligi kuanza upo njiani. Zipo timu ambazo zimeshuka na zipo ambazo zimepanda.

SOMA NA HII  ORODHA YA WACHEZAJI WAPYA WA SIMBA AMBAO HUENDA WAKAISHIA KUKAA BENCHI AU JUKWAANI

Ujumbe wangu kwa timu ambazo zimepanda daraja kwa msimu wa 2020/21 zikiwa na uhakika wa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22 zinapaswa zijipange kuleta ushindani.

Geita Gold na Mbeya Kwanza ziwatazame ndugu zao Gwambina na Ihefu namna mambo yalivyokwenda kwao. Pia waitazame Dodoma Jiji ambayo imefanya vizuri ndani ya ligi ikiwa ni msimu wake wa kwanza.

Hakuna timu ambayo inapenda kushuka lakini muhimu ni kuona kwamba kila timu inapata matokeo mazuri.Inawezekana kwa kujipanga na kutafuta matokeo bila kuchoka.

Ipo wazi ushindi unapatikana kwa kila timu ikijipanga na kufanya kazi kwa kushirikiana. Kwa muda ambao upo kwenye mashindano na namna ambavyo mtakuwa nyumbani basi ni muhimu kufanya vizuri.

Kwa zitakazoanza msimu ujao zinapaswa kuangalia kwamba kitu cha msingi ni kuanza kwa juhudi katika mzunguko wa kwanza mpaka ule wa pili.

Maisha ya kuwekeza nguvu mzunguko wa pili umekuwa ni tatizo kwa timu nyingi kushindwa kufanya vizuri mzunguko wa kwanza kwa kuwa wanaamini upo mzunguko wa pili.

Namna ambayvo timu zitaanza mzunguko wa kwanza maana yake ni kwamba zinakwenda kumaliza mzunguko wa pili kwa kasi ileile.

Tunaona kwamba Coastal Union na Mtibwa Sugar hizi zilianza kwa kusuasua mzunguko wa kwanza na zilikwenda na kasi hiyo mpaka mzunguko wa pili.

Ipo wazi kabisa na mwisho wa siku tumeona zilikuwa zinapambana katika mstari wa kushuka daraja lakini zimebaki bahati nzuri kwao.

Ni wazi kwamba kwa wakati ujao ikiwa zitaanza na kazi ileile kutakuwa na matokeo ya tofauti ambayo watayapata ndani ya uwanja.

Kote iwe ni Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili tunahitaji kuwe na ushindani kwa kila mmoja katika kutimiza majukumu yake.

Tunataka kuona kila timu inafanya maajabu na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote ambazo watacheza iwe nyumbani ama ugenini muhimu kupambana kupata matokeo.

Zilizopanda sasa ndani ya ligi ni muhimu kusahau maisha yao kule walikotoka na kuongeza nguvu huku kwenye maisha yao mapya ambayo wanayaanza.

Mashabiki wenu mtambue kwamba wanajua yapo matokeo matatu, kufungwa, sare na kushinda. Furaha yao kubwa ipo kwenye kushinda basi pambaneni kuwapa mashabiki kile ambacho wanahitaji.

Kila kitu ni kujipanga na inawezekana ikiwa kutakuwa na hesabu makini kwenye kutafuta matokeo ya mechi zote bila kuogopa.

Ni Azam FC ambao tayari wametinga hatua ya nusu fainali, KMKM na Yanga wao wanapambana kusaka nafasi ya kutinga hatua hiyo.

Jambo la msingi ni kuona kwamba kila mmoja anakuwa katika kusaka ushindi ndani ya uwanja.