Home Uncategorized SIMBA WACHEZEWA RAFU KAMA ZOTE NIGERIA, HESABU ZAO ZIPO NAMNA HII

SIMBA WACHEZEWA RAFU KAMA ZOTE NIGERIA, HESABU ZAO ZIPO NAMNA HII


WAWAKILISHI wa Tanzania, Simba wapo nchini Nigeria ndani ya mji wa Jos ambapo ndipo makazi ya wapinzani wao Plateau United ambao watakutana nao kesho Novemba 29 kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika huku ikielezwa kuwa wapinzani wao wamekuwa wakiwafanyia michezo ya kuwatoa kwenye mchezo.


Ikiwa chini ya Kocha Mkuu Svend Vandenbroeck, kesho ina kazi ya kusaka ushindi huku ikutana na kibarua kizito cha kupenya mbele ya wapinzani hao ambao wanaonekana kuwa ni watu wenye mipango mingi nje ya uwanja na ndani ya uwanja.


Habari zinaeleza kuwa baada ya kikosi cha Simba kutia timu jana, Novemba 27 mji wa Jos wakitokea Lagos kwenye hotel ambayo walifikia wahudumu waligomea wapishi maalumu wa Simba huku wakitaka watumike wale ambao wapo kwenye hotel zao.


Pia habari nyingine zinaeleza kuwa mbinu ya wapinzani wao ipo kwenye kuwapoteza Simba kwa kuwatoa nyota wake muhimu kwa kutumia vipimo vya Corona ili waukose mchezo huo.


Nyota ambao wanatajwa wapo kwenye hesabu hizo ni pamoja na Clatous Chama, Luis Miquissone, John Bocco na Rarry Bwalya.


Mratibu wa Simba, Abbas Gaza amesema kuwa kwa upande wa maandalizi wamekamilisha kwa asilimia 90 kinachosubiriwa ni masuala ya ndani ya uwanja, ambapo wana imani ya kupata matokeo chanya.

“Kila kitu kinakwenda kwa namna ambavyo kimepangwa, hatuna mashaka tunaamini kwamba yote ambayo yanatokeo huku tutapambana kupata matokeo,” .

SOMA NA HII  HAWA HAPA WAMESHIKILIA FUNGUO ZA USHINDI SIMBA V YANGA, TAIFA