Home Uncategorized EXCLUSIVE: GADIEL MICHAEL AFUNGUKA JUU YA KUSAINI SIMBA

EXCLUSIVE: GADIEL MICHAEL AFUNGUKA JUU YA KUSAINI SIMBA


Beki wa kushoto wa Yanga, Gadiel Michael,  amekanusha taarifa zilizozagaa kuwa amesaini mkataba na Simba na kwamba hajafanya mawasiliano yoyote na klabu hiyo.

Amesema suala la  kuongeza mkataba na klabu yake ya sasa  ya Yanga litakamilika siku chache zijazo baada ya kurejea kutoka kwenye mashindano ya ubingwa kwa nchi za Afrika (AFCON) yanayofanyika Misri.

Beki huyo amefunguka kufuatia kuzuka kwa tetesi ambazo hata wanachama na mashabiki wa Yanga zimewashtua.

Ikumbukwe hivi karibuni ilielezwa kuwa Yanga na Gadie wapo kwenye mazungumzo ya kumalizana na mchezaji huyo tayari kwa kumuongezea mkataba.

Licha ya Gadiel kukanusha, bado kuna taarifa za ndani kutoka Simba zinazoleleza kuwa mabosi wa klabu hiyo wapo kwenye mchakato wa kupata saini yake kuelekea msimu ujao.

SOMA NA HII  Okwi sio mchezaji wa Simba! Kaizer Chiefs yahusika