Home Habari za michezo ATUMIA MIL 56 KUNUNUA MBWA WA KULINDA MEDALI ZAKE ZA KOMBE LA...

ATUMIA MIL 56 KUNUNUA MBWA WA KULINDA MEDALI ZAKE ZA KOMBE LA DUNIA…

Martinez

Mlinda mlango wa Argentina na Aston Villa, Emiliano Martinez amemnunua Mbwa kwa kiasi cha pauni 20,000 (sawa na takribani Tsh milioni 56) kwa ajili ya kulinda nyumba na medali zake za kombe la Dunia zilizopo nyumbani kwake huko England.

Mbwa huyo ni aina ya Belgian Shepherd Malinois waliopitia mafunzo kwa ajili ya vikosi maalum.

Martinez alikuwa na kiwango bora kwenye fainal za kombe la dunia nchini Qatar, ambapo alifanikiwa kuiwezesha Argentina kushinda mchezo wa fainali dhidi ya Ufaransa.

Katika michuano hiyo, ambayo pia Martinez aliibuka golikipa bora wa mashindano, alipata umaarufu kwa kuokoa mikwaju ya penati katika hatua ya Robo Fainal na fainal.

Aidha, alimaliza michuano hiyo kwa kuacha kituko uwanjani ambapo wakati anakabidhiwa tuzo yake ya golikipa bora, alifanya ishara isiyo ya kiungwana , ambapo baadaye alikuja kuitolea maana , akisema kuwa ilikuwa ni ‘dongo’ kwa wafaransa.

SOMA NA HII  MO DEWJI AMWAGA MAMILIONI KWA WACHEZAJI SIMBA...WAPEWA ZAIDI YA MIL 600 ...CHAMA ,PHIRI WAONGOZA KWA MGAO MKUBWA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here