Home Azam FC KISA VIGEZO VYA FIFA……UWANJA WA CHAMAZI KUFUMULIWA UPYA….MPANGO MZIMA UKO NAMNA...

KISA VIGEZO VYA FIFA……UWANJA WA CHAMAZI KUFUMULIWA UPYA….MPANGO MZIMA UKO NAMNA HII…

MABOSI wa Azam FC wamepania kuuboresha uwanja wao ili kuendelea kukidhi vigezo vya Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA) sambamba Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Uwanja wa Azam Complex ni miongoni mwa viwanja bora ndani ya Afrika Mashariki.

Mhandisi wa uwanja huo, Victor Ndozero, amesema wanataka kuweka viti kwa mashabiki na kuondoa kabisa mbao ambazo zinakaliwa kwasasa.

Ndozero amesema viti hivyo tayari vipo bandarini na kilichobaki ni kuanza kuviweka ili wakidhi vigezo vya kimataifa.

“Tunaweka viti takribani 10,000 na hivi ni kwa mashabiki wanaokaa kwenye mabenchi kule ili kufikia levo ya Fifa na CAF,” amesema Ndozero na kuongeza;

“Viti hivyo vitakuwa na rangi ya machungwa, nyeusi, nyeupe na bluu, hakuna tena shabiki ambaye atakuwa amesimama.”

Ndozero amesema leseni ya uwanja wao inamalizika mwishoni mwa mwaka huu na wanataka itoke leseni nyingine ambayo itakuwa kubwa zaidi.

“Tunataka timu za Afrika nzima zikifungiwa viwanja vyao basi wafikirie kuja hapa Chamazi na ndio lengo letu.”

Victor ameongeza akisema utaratibu wa uwekaji viti hivyo utaanza pindi timu yao (Azam) itakapokuwa inacheza mechi za nje ya Chamazi.

“Ndani ya wiki mbili tunaweza kuweka viti 2000 hadi 3000 na mzunguko wa pili kabla haujaanza tutakuwa tumemaliza.”

Azam Complex ni uwanja wa sita wenye nyasi bandia nchini sambamba Kaitaba (Bukoba) na Uhuru (Dar), Nyamagana (Mwanza), Black Rhino (Karatu) na Majaliwa (Ruangwa).

Uwanja huo ulianza kutumika rasmi 2010 na kuingiza mashabiki 10,000

SOMA NA HII  YACOUBA : NAISUBIRI YANGA TU....SINA CHA KUPOTEZA...