Home Uncategorized ISHU YA MABADILIKO, SIMBA YAKUBALI KUFUATA TARATIBU ZA SERIKALI

ISHU YA MABADILIKO, SIMBA YAKUBALI KUFUATA TARATIBU ZA SERIKALI



SUALA la mabadiliko ndani ya Klabu ya Simba limeendelea kuleta picha mpya baada ya uongozi wa timu hiyo kujibu waraka kuhusu kukwama kwa mchakato wa mabadiliko.


Uongozi wa Simba umekubali kufuata taratibu zote zilizowekwa na Serikali ili kufanikisha mchakato wa mabadiliko.


Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Ushindani,(FCC) imekanusha taarifa inayodaiwa kutolewa na uongozi wa Simba iliyokuwa ikieleza kuwa tume hiyo inakwamisha mchakato wa uwekezaji ndani ya timu hiyo na badala yake umedai kuwa uongozi wa timu hiyo imekuwa ikijikwamisha yenyewe.


Tume hiyo ambayo ni taasisis ya Serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani Namba 8 ya 2003 (Sheria ya Ushindani) ili kusajiisha na kulinda ushindani wa biashara na kuwalinda walaji dhidi ya mienendo isiyo ya haki na ya kupotosha. 

Baada ya waraka huo leo Simba imeweka wazi kuwa wapo tayari kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali ili kukamilisha mchakato wa mabadiliko. 


Taarifa yao ipo namna hii:-


SOMA NA HII  MBAO YAJIPIGIA BAO 1-0 POLISI TANZANIA