Home KMC FC MIRAJ ATHUMAN MALI YA KMC

MIRAJ ATHUMAN MALI YA KMC


KIUNGO mshambuliaji Miraj Athuman ambaye alikuwa nyota wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes sasa ni rasmi kuwa atakuwa mali ya KMC.

Nyota huyo hakuwa kwenye nafasi nzuri msimu uliopita kutokana na kukosa nafasi kikosi cha kwanza pia majeraha ya mara kwa mara ilikuwa sababu ya nyota huyo kujenga ushkaji na benchi.

Anaungana na Faroukh Shikalo ambaye huyu alikuwa anakipiga Yanga msimu uliopita na kwa sasa atakuwa ndani ya KMC.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa ni mapendekezo ya benchi la ufundi usajili wao.

SOMA NA HII  KIFAA KIPYA YANGA CHAANZA NA MKWARA WA KUFA MTU...AJITOFAUTISHA NA WENZAKE...