Home kimataifa HIZI HAPA ZILITUNGULIWA MABAO MENGI NA MESSI

HIZI HAPA ZILITUNGULIWA MABAO MENGI NA MESSI

 


LIONEL Messi raia wa Argentina amefunga jumla ya mabao 76 katika timu yake ya taifa kwenye jumla ya mashindano yote huku ile timu ya taifa ya Ecoador ikiwa imefungwa mabao mengi na nyota huyo ambayo ni sita.

Timu inayofuatia kwa kufungwa mabao mengi baada ya Ecoador ni timu ya taifa Borivia, Brazil,Chile,Paraguay na Uruguay hizi zote alizitungua mabao matanomatano.

Amecheza jumla ya mechi 151 sawa na dakika 13,590, ambapo za kirafiki alicheza jumla ya mechi 47 na alitupia mabao 34, Copa America alicheza mechi 34 alitupia mabao 13 katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia alicheza mechi 51 na mabao aliyotupia ni 23.

Rekodi zinaonyesha kuwa hat trick yake ya kwanza akiwa katika timu ya taifa ya Argentina alifunga mbele ya Switzerland na ilikuwa ni mwaka 2012.

Kwenye mechi zake za Kombe la Dunia alicheza mechi 19 na mabao aliyofunga ilikuwa ni 6 ambapo alifunga mara ya kwanza ilikuwa ni 2006, mabao manne alitupia 2014 na alitwaa tuzo ya kiatu bora cha ufungaji na moja alifunga 2018.

Raia huyo wa Argentina jumla ametupia jumla ya hat trick sita kwenye timu yake hiyo ya taifa. Jumla ametupia mabao 23 katika mashindano hatua za kufuzu Kombe la Dunia na kumfanya.

 

SOMA NA HII  AISEE!! HUYU SAMATTA WAMUACHE...WAZUNGU WAPASUKA VICHWA WAMUOGOPA