Home kimataifa AISEE!! HUYU SAMATTA WAMUACHE…WAZUNGU WAPASUKA VICHWA WAMUOGOPA

AISEE!! HUYU SAMATTA WAMUACHE…WAZUNGU WAPASUKA VICHWA WAMUOGOPA

Habari za Michezo

Nyota ya nahodha wa timu ya Taifa Tanzania na mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta imeendelea kung’aa baada ya juzi kufunga bao moja kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Charleroi kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Ubelgiji.

Samatta huu ni muendelezo wake wa kutupia mfululizo baada ya mchezo uliopita dhidi ya Anderlecht alifunga bao moja wakati timu yake (Genk) ikishinda 5-2.

Nahodha huyu amefunga mabao sita kwenye kikosi cha Genk huku kinara wa mabao kwenye timu yao akiwa ni Paul Onuachu ambaye alifunga mabao 15 na ameondoka kwa sasa anakipiga Ligi ya Uingereza (Southampton).

Mabao ya Samatta kwenye mechi mbili mfululizo yamechangia Genk imalize ligi ikiwa na pointi 75 ikiwa kinara kwenye msimamo sawa na Union Saint-Gilloise na kwenda kwenye mchujo wa ubingwa hukuu ikiendelea kuongoza Ligi.

Genk kama ikifanikiwa kuchukua ubingwa basi itacheza Ligi ya Mabingwa kwa kuanzia hatua ya mchujo lakini kama ikimaliza nafasi ya pili basi itacheza kwenye raundi ya pili.

Samatta kama timu hiyo itachukua ubingwa basi itakuwa ni mara ya pili akichukua ubingwa baada ya msimu wa 2018-2019 kufanya hivyo huku yeye akifunga mabao 20.

Genk inaingia kwenye mchujo wa ubingwa ikiwa na pointi 38 baada ya pointi ilizomaliza nazo ligi kugawanywa mara mbili (75) lakini bado imeendelea kufungana kwa pointi na Union Saint- Gilloise huku nafasi ya tatu ikiwa ni Royal Antwerp (36) na Club Brugge (30).

Ili Genk ihakikishe inachukua ubingwa inatakiwa kwenye mechi sita ambazo itacheza basi ihakikishe inajikusanyia pointi za kutosha na kuwaacha mbali wapinzani wao wengine.

Genk itaanza kutupa karata yake ya kwanza kwenye mchujo wa ubingwa ikiwa nyumbani dhidi ya Club Brugge, Aprili 30 kisha itakuwa ugenini dhidi ya Royal Antwerp Mei 7.

Mechi zingine ni Union Saint-Gilloise va Genk (Mei 14), Genk vs Union Saint-Gilloise (21 Mei), Club Brugge vs Genk (Mei 28) na Genk vs Atwerp (Juni 4).

SOMA NA HII  BENCHIKHA AFUNGUKA JINSI WATAKAVYOCHUKUA POINTI TATU MBELE YA WYDAD