Home Habari za michezo BAADA YA KUSAJILIWA CHELSEA…AUBAMEYANG AIPIGA ‘DONGO LA KARNE’ ARSENAL…

BAADA YA KUSAJILIWA CHELSEA…AUBAMEYANG AIPIGA ‘DONGO LA KARNE’ ARSENAL…


Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang amesema bado kuna mambo hakuyakamilisha wakati anaondoka Ligi Kuu England ambayo anahitaji kuyakamilisha wakati huu.

Aubameyang ametoa kauli hiyo baada ya kukamilisha uhamisho wake wa kutoka FC Barcelona kwenda Chelsea kwa dau la pauni milioni 10.3 ikiwa ni mara ya pili anarejea kwenye Ligi ya EPL baada ya awali kuitumikia Arsenal.

Aliondoka Arsenal Januari mwaka jana akiwa amefunga magoli 92 kwenye mechi 163 kama mchezaji huru baada ya kutofautiana na kocha wa klabu hiyo Mikel Arteta.

Akizungumza baada ya kutambulishwa na kupewa jezi nzito ya namba tisa, Aubameyang amesema “kuna mambo ambayo sikuyatimiza wakati naondoka hapa England, nahitaji kuyafanya hapo sasa”, kauli hiyo ni kama ahadi kwa mashabiki wa Chelsea.

Anarudi England, Chelsea na kuungana na kocha Thomas Tuchel amesema ambaye walifanya kazi pamoja kwenye kikosi cha Borrusia Dortmund kwenye kipindi cha mwaka ‪2015 – 2017‬.

SOMA NA HII  KUHUSU UKAME WA MAGOLI KWA KIBU....UKWELI UNAOPASWA KUJUA HUU HAPA....