Home news PABLO ALETA BALAA JIPYA SIMBA…HITIMANA KAMA KAWA HAKOSI NENO…AFUNGUKA KUHUSU USHIRIKIANO..

PABLO ALETA BALAA JIPYA SIMBA…HITIMANA KAMA KAWA HAKOSI NENO…AFUNGUKA KUHUSU USHIRIKIANO..


KOCHA Mkuu wa Simba, Mhispania, Franco Pablo, amekuja kivingine katika kikosi chake akimtaka kila mchezaji kufanya mazoezi binafsi.

Hiyo ni katika kuhakikisha kila mchezaji anakuwa na fiziki ya kutosha ndani ya uwanja wakati kikosi hicho kikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Wakati kocha huyo akipambania fiziki kikosini kwake, tayari KOCHA mpya wa viungo wa Simba, Don Daniel De Castro, ameanza na mkwara mzito kwenye majukumu yake ndani ya Simba, baada ya juzi Jumanne kuwaweka kikao kizito mastaa wa kikosi hicho.

Raia huyo wa Hispania, amekuja kuchukua nafasi ya Kocha Mtunisia, Adel Zrane ambaye alisitishiwa mkataba wake Oktoba 26, mwaka huu.

Juzi Jumanne, De wa timu hiyo umemleta kocha mpya wa viungo kutoka Hispania, Don Daniel De Castro.

Mmoja wa viongozi kutoka ndani ya Benchi la Ufundi la Simba, ameliambia Spoti Xtra kuwa mazoezi ya timu pekee hayatoshi kwa mchezaji, hivyo kocha amesisitiza ni lazima kwa kila mchezaji kufanya mazoezi ya ziada.

Kiongozi huyo alisema Pablo ndani ya wakati atafanya mambo mawili ambayo kutengeneza mfumo kwa kuwapa mbinu za uchezaji na fitinesi.

Aliongeza kuwa, Castro alianza kazi rasmi katika mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterani, Dar, ambapo kwa muda wote alionekana kufuatilia kwa ukaribu namna ambavyo wachezaji walikuwa wakifanya programu walizopewa.

Katika kuonesha kuwa alikuwa akiwafuatilia kwa umakini, mara tu baada ya mazoezi hayo, alikuwa akizungumza na mchezaji mmoja mmoja huku akitumia muda mwingi kuzungumza na Gadiel Michael na Kibu Denis.

Kocha huyo amepanga kulisisitiza hilo kwa wachezaji baada ya kuona upungufu huo katika mchezo wa kirafiki waliocheza dhidi ya Cambiaso Academy, hivi karibuni.

“Kocha ndani ya wiki hii ametumia muda mwingi kukiangalia kikosi chake mazoezini na kuomba mchezo mmoja wa kirafiki maalum kwa ajili ya kuangalia upungufu wa wachezaji wake.

“Kikubwa alichogundua ni timu kukosa umakini katika kufunga mabao na hilo limetokana na kukosa kujiamini na fitinesi ndogo.

SOMA NA HII  MO DEWJI AWAPASUKIA SIMBA...ASEMA KUWEKEZA KWENYE TIMU HIYO NI HASARA TUPU...AMTAJA TRY AGAIN...

“Haraka akaagiza kila mchezaji kufanya mazoezi ya binafsi nje ya timu kwa ajili ya kuongeza fiziki na hilo siyo ombi ni amri kila mmoja lazima afanye kwa lengo la kutengeneza utimamu wa mwili,” alisema kiongozi huyo.

Akizungumzia hilo, Kocha Msaidizi wa Simba, Thiery Hitimana raia wa Rwanda, alisema: “Kocha mkuu amesisitiza nidhamu, umoja na ushirikiano katika timu pamoja na kila mmoja kufuata maelekezo yake ambayo amekuwa akiyatoa mazoezini.”