Home news KISA KUPOTEZA UBINGWA WA MAPINDUZI..NABI AFURA KWA HASIRA YANGA…ATOA AMRI HII MPYA…

KISA KUPOTEZA UBINGWA WA MAPINDUZI..NABI AFURA KWA HASIRA YANGA…ATOA AMRI HII MPYA…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameweka wazi kuwa hataki kuona nyota wake wakifanya makosa ya kupoteza nafasi yao ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na kuwataka kuhakikisha wanacheza kila mchezo ulio mbele yao kama fainali.

Yanga ambao ni vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara, hawakuwa na matokeo mazuri katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu, kufuatia kuvuliwa kombe hilo katika hatua ya nusu fainali walipocheza dhidi ya Azam.

Juzi Jumapili Nabi alikiongoza kikosi cha  Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ugenini, pale walipovaana dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli mbili bila.

Akizungumza na gazeti la Championi Jumatatu, kocha Nabi alisema: “Tuliweka wazi tangu mwanzoni mwa msimu huu kuwa tunahitaji kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao hatujashinda kwa kipindi cha miaka minne sasa, najua kuna namna wachezaji, viongozi na hata mashabiki hawajaridhishwa kuona tumepoteza Kombe la Mapinduzi.

“Lakini hatupaswi kusalia katika kuwazia hayo kwa kuwa tayari yamepita, jambo la muhimu ambalo nimewaambia wachezaji wangu ni kuwa lazima tuhakikishe tunauchukulia kila mchezo kwa uzito wake na kucheza kama fainali ikiwa tunahitaji kushinda ubingwa.”

SOMA NA HII  USHIRIKINA WAIPONZA TIMU YA MASHUJAA FC, WAPIGWA FAINI HII