Home Habari za michezo ZA NDAANI KABISA….KOCHA WA ZAMANI AL AHLY AITAKA SIMBA…ATUMA MAOMBI RASMI …

ZA NDAANI KABISA….KOCHA WA ZAMANI AL AHLY AITAKA SIMBA…ATUMA MAOMBI RASMI …

 


Taarifa zilizotufikia kutoka vyombo vya habari nchini Afrika Kusini zinasema aliyekuwa kocha msaidizi wa Al Ahly, Cavin Johnson ametuma maombi ya kuajiriwa kama Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Sc ambayo kwa sasa iko chini ya kocha wa muda Juma Mgunda baada ya kuachana na Kocha wake, Zoran Manojlović Maki.

Johnson ambaye ni raia wa Afrika Kusini aliondoka Ahly kama msaidizi wa Pitso Mosimane, Septemba mwaka jana, ingawa haikufahamika kwa nini aliihama klabu hiyo ambayo ilikuwa imetoka kushinda Ligi ya Mabingwa ya CAF mwezi Julai baada ya kuifunga Kaizer Chiefs.

Johnson akiwa Kama kocha msaidizi wa Al Ahly chini ya Pitso Mosimane alifanikiwa kutwaa Ligi ya Mabingwa mara mbili, CAF Super Cup, Kombe la Misri na kunyakua medali ya shaba ya Klabu Bingwa wa Dunia (FIFA Club World Cup) mara mbili mfurulizo.

Kwa upande wa Simba mpaka sasa bado hawajatoa tamko lolote iwapo wameshapokea wasifu ama maombi ya makocha kutoka nje ama ndani ya nchi licha tu ya kusema kwamba wanafanya mawasiliano na makocha watatu walioingia kwenye kinyang’anyiro cha awali ambapo Zoran alipata nafasi ya kuajiriwa na miamba hao wa soka Tanzania.

SOMA NA HII  CV ZA KIPA MPYA WA SIMBA NI HATARI, MBRAZILI ANABALAA HUYU