Home Habari za michezo PAMOJA NA KUKOSA MAGOLI YA WAZI JANA….STRAIKA MZUNGU WA SIMBA AZIDI KULIKOROGA…ATOA...

PAMOJA NA KUKOSA MAGOLI YA WAZI JANA….STRAIKA MZUNGU WA SIMBA AZIDI KULIKOROGA…ATOA UJUMBE HUU MKALI…


Kikosi cha Simba kimepoteza mchezo wa mwisho wa kirafiki kwenye kipindi cha mapumziko ya FIFA kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Arta Solar 7 ya Djibouti mchezo uliopigwa dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Arta Solar wanakamilisha ziara ya mechi zao za kirafiki nchini baada ya awali kufungwa 3-0 na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na sasa wanarejea nyumbani.

Bao la ushindi kwa timu hiyo limefungwa dakika za mwishoni mwa kipindi cha pili jambo ambalo limewanyima nafasi ya kubakia hapa kundelea kuwepo.

Pamoja na kwamba Simba wamepoteza jambo ambalo ni kawaida kwa mpira wa kisasa, lakini uwezo wa mshambuliaji mpya wa Simba Dejan Geirgejevic umekuwa maji kupwa, maji kujaa.

Maneno hayo yanakuja kufuatia kupoteza nafasi mbili muhimu kwenye nafasi ambayo walidhania isingekuwa rahisi mfano Meddie Kagere kukosa maeneo hayo.

Sasa, maneno hayo pia ni kama yamemudhi Dejan, kwani kupitia ukurasa wake wa instagram amekomenti kwenye ujumbe wa shabiki wake kwa kusema kuwa huu ni uchizi, na hii ni mara baada ya jana kutwa mzima alikuwa akikejeliwa.

SOMA NA HII  MGUNDA : SIMBA TUNAKAZI KUBWA....AFUNGUKA NAMNA UGUMU ULIVYO...