Home Habari za michezo BENCHIKHA AFUNGUKA JINSI WATAKAVYOCHUKUA POINTI TATU MBELE YA WYDAD

BENCHIKHA AFUNGUKA JINSI WATAKAVYOCHUKUA POINTI TATU MBELE YA WYDAD

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amesema anafahamu mchezo wa leo dhidi ya Wydad AC itakuwa ngumu lakini ataingia kwa umakini mkubwa.

Amesema, mchezo huo unahitaji nguvu ya pamoja ili kuhakikisha wanapata ushindi ili waweze kusonga mbele.

“Mechi hii ni muhimu kwetu kupata ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele hatua inayofuata, tunatakiwa kuwa na nguvu ya pamoja na umakini mkubwa, wachezaji wangu wanao uwezo wa kulitimiza hili na wanajiamini kwa ajili ya kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Wydad,” alisema Benchikha.

SOMA NA HII  SHINDA MPAKA MARA 270 YA DAU LAKO KUPITIA SLOT YA KIJANJA YA BLACKJACK NDANI YA MERIDIANBET..