Home Habari za michezo A-Z JINSI SIMBA ILIVYOIFINYANGA RUVU SHOOTING JANA…BOCCO ATOA GUNDU LA MIEZI TISA…

A-Z JINSI SIMBA ILIVYOIFINYANGA RUVU SHOOTING JANA…BOCCO ATOA GUNDU LA MIEZI TISA…


BAADA ya siku 294 ambazo ni sawa na miezi tisa na siku 21 hatimaye kinara wa mabao msimu uliopita John Bocco, amefunga bao lake la kwanza kwenye Ligi kuu msimu wa 2021/2022.

Bocco ameifungia Simba bao lake la kwanza na la tatu kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting wakishinda mabao 4-1 kwenye uwanja wa Mkapa.

Mchezaji huyo mara ya mwisho kufunga bao kwenye Ligi kuu ni Julai 18 2021 dhidi ya Namungo.

Bao la kwanza la Simba lilifungwa dakika ya 40 kipindi cha kwanza na Kibu Denisi, pili lilifungwa na Rally Bwalya dakika ya 67, wakati Bocco akifunga dakika ya 82.

Baada ya bao hilo la Bocco Ruvu Shooting walijibu mashambulizi ya haraka na kupachika bao la kufutia machozi dakina ya 83 likifungwa na Haruna Chanongo.

Dakika mbili baadaye Simba walipata bao la nne kupitia kwa beki Henock Inonga dakika ya 85 ambalo lilikuwa ni la nne kwa Simba na kufikisha pointi 46 ambazo zinawafanya waendelee kubaki nafasi ya pili.

Kipindi cha pili timu zote zilicheza kwa kujilinda huku zilotafuta upenyo wa kufunga Simba wakihitaji kuongeza bao na Ruvu wakitafuta nafasi ya kusawazisha.

Simba dakika ya 67 walifanya mabadiliko kwa kumtoa Kagere na nafasi yake ilichukuliwa na John Bocco pia alitoka Banda na nafasi yake ilichukuliwa na Yusuf Mhilu.

SOMA NA HII  NABI:- AZIZ KI HAKUCHEZA KWA MASLAHI YA YANGA...HAKUWA BORA KWANGU ...