Home Uncategorized MKUDE; WENGI WANASEMA JUU YANGU,SIWEZI KUWAZUIA

MKUDE; WENGI WANASEMA JUU YANGU,SIWEZI KUWAZUIA


JONAS Mkude, kiungo mkabaji ndani ya klabu ya Simba amesema kuwa watu wengi wanaomsema vibaya hawezi kuwazuia kwa kuwa wameamua kumwandama bila kujua kinachomsumbua.

Mkude amesema kuwa kushindwa kwake kujiunga ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hivi karibuni kumeibua maneno mengi kwa kila mmoja kutaja sababu anazozijua.

“Wengi wamesema vile ambavyo wanajua wao ila ukweli unabaki kwamba mimi ni binadamu na matatizo yananikuta pia, haina maana kwamba sipendi kutimiza majukumu yangu hapana kuna wakati mwingine nakwama kutokana na matatizo ambayo ninayapata,” amesema.

Kambi ya Stars iliyokuwa inajiaandaa na michuano ya CHAN ilivunjwa hivi karibuni kwa ajili ya kuzuia maambukizi zaidi ya Corona, Mkude alichaguliwa kujiunga na kambi hiyo kabla ya kuvunjwa ila hakuripoti mpaka kambi ilipovunjwa.

SOMA NA HII  BAADA YA SAMATA KUTUA ASTON VILLA, MTANZANIA MWINGINE ARITHI NAFASI YAKE GENK