Home Uncategorized WAKALI WA KUTUPIA MABAO 11 WOTE NI WAZAWA, WAWILI WANA KITAMBAA CHA...

WAKALI WA KUTUPIA MABAO 11 WOTE NI WAZAWA, WAWILI WANA KITAMBAA CHA UNAHODHA



KWA wachezaji walio kwenye mwendo wa kutupia mabao 11 ni watatu na wote ni wazawa ambapo wawili kwenye timu zao ni manahodha.

Paul Nonga anakipiga ndani ya Lipuli na ni nahodha pia ana mabao 11 na pasi nne za mabao. Timu yake jumla imefunga mabao 35 ikiwa imecheza mechi 29.

Reliants Lusajo anakipiga ndani ya Namungo ametupia mabao 11 ni nahodha wa Namungo. Timu yake imefunga jumla ya mabao 34 ikiwa imecheza mechi 28

Mzawa mmoja ambaye ni Yusuph Mhilu ametupia mabao 11 huku timu yake ikiwa imefunga jumla ya mabao 36 ikiwa imecheza mechi 29.

Licha ya kutupia pia ana pasi mbili za mabao ndani ya Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  MABINGWA WA LIGI KUU BARA WATAJA WANAOSTAHILI KUSHUKURIWA KWA TAJI LAO LA 21, WAKABIDHIWA KOMBE LINDI