Home Uncategorized ASTON VILLA INA KAZI YA KUFANYA LIGI KUU ENGLAND ITAKAPOREJEA

ASTON VILLA INA KAZI YA KUFANYA LIGI KUU ENGLAND ITAKAPOREJEA

ASTON Villa, klabu anayokipiga Mbwana Samatta nahodha wa Tanzania ndani ya Ligi Kuu England imejikusanyia pointi 25 baada ya kucheza mechi 28.

Villa imefunga jumla ya mabao 34 ambapo moja kati ya hayo Samatta naye alipachika bao moja pia.

Imeshinda mechi 4 na kupoteza mechi 16 na kulazimisha sare 7 ndani ya Ligi Kuu England ipo nafasi ya 19 ina kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi zake zlizobaki ili kujinasua kutoka hatari ya kushuka daraja.


Samatta alijiunga na Klabu ya Aston Villa akitokea timu ya KRC Genk ambapo mpaka sasa amecheza mechi nne za Ligi Kuu England. 

Kwa sasa ligi ya England imesimama na inatarajiwa kurejea Aprili 30 kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

SOMA NA HII  MASHINE MPYA 10 ZA DODOMA FC HIZI HAPA