Home Habar za Usajili Simba MASHINE TANO SIMBA KUTUA MISRI LEO…VYUMA VITATU VIPYA KUTAMBULISHWA KININJA…SAJILI ZOTE...

MASHINE TANO SIMBA KUTUA MISRI LEO…VYUMA VITATU VIPYA KUTAMBULISHWA KININJA…SAJILI ZOTE ZIMETIKI…


Kikosi cha Simba tayari imeshatua hapa Ismalia na kufikia hoteli ya kishua ya Mercure Ismailia Forsan Island tayari kwa kambi ya wiki tatu kabla ya kurejea Tanzania Agosti 5. Lakini kama hukumbuki ni kwamba sajili zote ambazo tulikudokeza kuhusu Simba zimetiki.

Kuna mafundi wengine watakuja moja kwa moja hapa Ismailia na hawajafikiwa zamu yao ya kutangazwa kwenye ule usajili wa saa 7 mchana.

Yumo beki wa zamani wa Al Hilal ya Sudan, Mohammed Ouattara na kiungo mshambuliaji, Nelson Esor Okwa kutoka Nigeria.

Kundi la kwanza limetua hapa na taarifa za uhakika ni kwamba kambi ya Simba itakuwa na watu 48. Benchi la ufundi watu 12 akiwamo kocha mkuu, Zoran Maki, wachezaji 30 na viongozi sita.

Mbali na Maki, benchi hilo lina wasaidizi  ambao ni kocha wa makipa, Mohamed Haniched kutoka Algeria na kocha wa viungo Mtunisia, Karim Sbai ambao wataungana na mzawa Selemani Matola.

Pia wamo mratibu Abbas Suleiman, meneja Patrick Rweyemamu, mtaalamu wa misuli, Fareed Cassim, mtaalamu wa kuchambua video, Culvin Mavunga, daktari Edwin Kagabo, ntunza vifaa, Hamisi Mtambo na mpishi Samwel Cyprian.

Kwa upande wa viongozi kuna watu sita akiwamo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’, Mjumbe wa Bodi wa Wakurugenzi, Mulamu Nghambi, Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez, Meneja wa Habari, Ahmed Ally, Msimamizi wa Maudhui, Ally Shantry na Crescentius Magori.

Kundi la mwisho la Simba ndani ya Misri linawajumuisha wachezaji 25 ambao ni Benno Kakolanya, Ally Salim, Shomary Kapombe, Israel Mwenda, Victor Akpan, Gadiel Michael, Habib Kyombo, Moses Phiri na Joash Onyango.

Wachezaji wengine, Henock Inonga, Sadio Kanoute, Nassoro Kapama, Clatous Chama, John Bocco, Jimyson Mwanuke, Meddie Kagere, Peter Banda, Augustine Okrah, Pape Sakho, Taddeo Lwanga, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Chriss Mugalu.

Kwenye orodha ya wachezaji wapya wapo Okwa na Ouattara ambao muda wowote kuanzia leo watatambulishwa. Yusuph Mhilu hayupo kwenye orodha na inaelezwa huenda asiwepo kwenye kikosi cha Simba msimu ujao kwani amepata ofa mbili kutoka Zambia pamoja na Afrika Kusini.

SOMA NA HII  NYOTA WA YANGA AMISS TAMBWE KURUDI BONGO

Wachezaji watano waliopo kambi ya Taifa Stars, Aishi Manula, Mohammed Hussein, Mzamiru Yassin, Kibu Denis na Kennedy Juma watajumuika na wenzao kukamilisha idadi ya wachezaji 30 wa Simba kwa msimu huu.

Habari za uhakika zinasema kwamba Ceasar Manzoki huenda akakosa kambi hiyo kama atashindwa kupata vibali vyake kwa wakati kwani mpaka sasa klabu yake ya Vipers ya Uganda inadai ina mkataba naye ambao Simba inapaswa kwenda mezani na mkwanja wayajenge.

Rekodi zinaonyesha hii si mara ya kwanza Vipers kuingia kwenye mzozo na wachezaji kwani hata katika miaka ya hivi karibuni kuna wachezaji walienda kuwashtaki kwenye Shirikisho na sheria zikawakuta hawana hatia wakaondoka bure. Lakini Mwanaspoti linajua chochote kinaweza kutokea kabla ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 31.

Mapema wakati kikosi kikiondoka jijini Dar es Salaam, kocha msaidizi, Seleman Matola alifichua msafara wao utakuwa na makundi matatu, wale walioondoka juzi, kundi la pili litafuata la wachezaji waliochelewa kupata viza na kundi la tatu ni wale waliopo Taifa Stars.

“Haina jinsi ni changamoto ambayo tunapambana nayo ila naamini tutakuwa na kambi nzuri kwa kila mchezaji kutumia vizuri muda ambao atapata kwani huku tutacheza na mechi ya kirafiki tena ndani ya wiki ya kwanza,” alisema Matola na kuongeza;

“Kuhusu Mhilu kuna mambo yake na uongozi anayaweka sawa ndio maana kwenye timu hayupo ila baada ya kumalizika ndio tutafahamu kama msimu ujao tutakuwa naye au kuna mahali pengine atakwenda.”