Home news NYOTA WA YANGA AMISS TAMBWE KURUDI BONGO

NYOTA WA YANGA AMISS TAMBWE KURUDI BONGO


 IMEELEZWA kuwa nyota wa zamani wa kikosi cha Yanga, Amiss Tambwe yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya kikosi cha DTB kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Tambwe alisepa ardhi ya Tanzania baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo zama hizo Mwinyi Zahera kutokubali uwezo wake.

Msimu anapoepa Tanzania 2017/18 alitupia jumla ya mabao 12 ambapo alifunga mabao 8 kwenye ligi na manne kwenye Kombe la Shirikisho.

Kwa sasa mchezaji huyo yupo huru hivyo akikamilisha dili la kujiunga na timu hiyo atakuwa kwenye mkataba mpya.

Hivi karibuni, Tambwe alisema kuwa yupo tayari kucheza Tanzania ikiwa atapata ofa nzuri kwa kuwa bado uwezo anao.

SOMA NA HII  PAMOJA NA MOSES PHIRI KUTAKATA KIMATAIFA...FEI TOTO AIBUKA MBABE KWA HILI...ISHU IKO HIVI...