Home Uncategorized JOSE MOURINHO ATOA SAPOTI KWA WAZEE WALIOPO KARANTINI

JOSE MOURINHO ATOA SAPOTI KWA WAZEE WALIOPO KARANTINI


JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Tottenham ametoa msaada wa chakula kwa wazee wa kituo cha Your Door Step kilichopo Enfield.
Kocha huyo wa Tottenham aliwatembelea watu wa kituo hicho kilicho karibu na sehemu ya kufanyia mazoezi ya timu yake ya Spurs ambapo aliwapelekea chakula na vitu vingine muhimu ikiwa ni sehemu ya msaada kwa jamii inayomzunguka.
Mourinho amesema kuwa lengo lake ilikuwa ni kuwasaidia wazee hao wanaoishi kwenye kituo hicho cha Love Your Door Step na kuwataka wengine kufanya hivyo pia kwa ajili ya kutoa mchango wao.
Wazee hao wameshauriwa kukaa karantini kwa muda wa wiki 12 ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.
“Nipo hapa kwenye kituo cha Love Your Door Step Enfield kwa ajili ya kuchangia kile ambacho ninacho ambacho ni chakula na unaweza kujitoa pia kwa ajili ya kuwapa msaada iwe ni chakula, fedha ama kujitoa kwa ajili yao,” amesema kupitia video iliyotumwa na Love Your DoorStep kwenye akaunti ya Twitter.
SOMA NA HII  TUIPE SAPOTI STARS, MZUNGUKO WA SITA UTUZINDUE KIUSHINDANI