Home Uncategorized CHAMA AKINUKISHA NDANI YA SIMBA, YUPO ZAKE ZAMBIA KWA SASA

CHAMA AKINUKISHA NDANI YA SIMBA, YUPO ZAKE ZAMBIA KWA SASA


IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba, Clatous Chama amegoma kuongeza kandarasi ndani ya klabu yake hiyo kwa ajili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Uongozi wa Simba ulifanya mazungumzo na nyota huyo ambaye mkataba wake unatarajia kumeguka mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo aligoma kuongeza kandarasi na kuwataka mabosi wa Simba wasubiri kwanza mpaka pale mkataba utakapomeguka jambo lililoibua wasiwasi kwa viongozi hao kuhofia kuzidiwa ujanja na klabu nyingine.

Kwa sasa Chama hayupo Bongo yupo zake nchini Zambia baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona. 


“Kuna uwezekano mkubwa Chama kuhama klabu ya Simba mwishoni mwa msimu hii ni baada ya kugomea mkataba mpya aliopewa kwa ajili ya kusaini baada ya ule wa miaka miwili kumalizika mwishoni mwa msimu huu. 

“Chama ameomba kusaini mkataba huo baada ya ligi kumalizika, kitu ambacho viongozi hawataki kuskia Kwa hofu kuwa nyota huyo anaweza kuibukia klabu nyingine,” kilieleza chanzo.

Katibu Mkuu wa Simba, Dr.Arnold Kashembe amesema kuwa hilo ni suala la kiutawala hawezi kulizungumzia kwa kuwa muda wa usajili bado.

SOMA NA HII  AZAM FC WAIKOMALIA KAGAME, SASA NGUVU ZAO WAMEWEKEZA HUKU