Home Yanga SC NYOTA WAWILI YANGA HATIHATI KUIKOSA MWADUI KISA UTOVU WA NIDHAMU

NYOTA WAWILI YANGA HATIHATI KUIKOSA MWADUI KISA UTOVU WA NIDHAMU


 NYOTA wawili wa Yanga wamekumbwa na hali ya kufanana kwa kuondolewa kwenye kikosi kwa kosa la utovu wa ndhamu.

Leo Mei 25, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mwadui FC huku ikitarajiwa kuwakosa nyota wawili ambao wamesimamishwa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Mchezaji wa kwanza kusimamishwa kwa kosa la utovu wa nidhamu ni nahodha Lamine Moro ambaye alisimamishwa wakati timu ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa Moro alisimamishwa kutokana na Nabi kueleza kwamba alikuwa na makosa ya kinidhamu.

Nyota mwingine ambaye ametajwa kuwa amesimamishwa na Nabi kutokana na utovu wa nidhamu ni kipa namba moja Metacha Mnata.

Mnata anatajwa kusimamishwa na Nabi kwa kosa la utovu wa nidhamu hivyo naye huenda ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Mwadui FC. 

Mnata ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo aliibuka hapo akitokea Klabu ya Mbao ambayo kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza lakini msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Pili kwa sababu imeshuka pia daraja.

SOMA NA HII  ALICHOKISEMA INJINIA HERSI BAADA YA YANGA KUPANGWA NA AL AHLY LIGI YA MABINGWA...