Home news ISHU YA UWANJA MPYA SIMBA NA AHADI YA MO YACHUKUA SURA...

ISHU YA UWANJA MPYA SIMBA NA AHADI YA MO YACHUKUA SURA MPYA…’KIGOGO’ AFUNGUKA YA NDANI….


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’

UONGOZI wa juu wa Klabu ya Simba umepanga kukutana ndani ya siku mbili hizi ili kujadili na kupanga wapi wataanzia mpango wa kujenga uwanja wao wa nyumbani kama alivyoshauri mwekezaji,Mohamed Dewji (Mo Dewji).

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ akieleza kuwa kitendo cha Mo kusema atatoa Bil 2 kwa ajili ya kujenga uwanja siyo cha kulazia damu na wanatakiwa kukutana haraka kuanza kutekeleza.

Mo, kupitia ukurasa wake wa Instagram juzi aliandika kuwa: “Nimepokea maoni mengi ya Wanasimba wenzangu wakishauri tujenge uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili tufanikishe ujenzi huo.

“Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili. Naomba Bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji.

“Kwa kuanza naahidi kuchangia Tsh. 2 bilioni. Nawaomba Wanasimba tuchangie sote.” Akizungumzia ombi la Mo la kuitaka Bodi ya Simba ikutane na kuja na utaratibu wa kuanza zoezi hilo, Try Again alisema: “Kimsingi neno lake limekuwa kubwa kwa Wanasimba wote na sisi kama bodi tutakutana haraka ili kuweza kujadili suala hilo.

“Binafsi nilikuwa natamani sana kuona siku nikiwa naondoka Simba niwe nimeacha alama ambayo itafanya nikumbukwe na Wanasimba wote, hivyo kwa haraka sana tutaanza mchakato baada ya viongozi kukubaliana.”

Kauli ya Mo ilikuja baada ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kudai kuwa amezuiwa kuingia Uwanja wa Mkapa kushuhudia mechi ya Simba dhidi ya Yanga

SOMA NA HII  SIMBA YATOA TAMKO BAADA YA KUNYOOSHWA KWA MKAPA